Skip to main content
x
Maadhimisho ya siku ya wanawake na ukombozi wa wazalishaji wadogo.

Historia ya siku ya Wanawake duniani inaonesha kuwa tarehe 8 Machi ilichaguliwa kusherehekea siku ambayo wanawake katika Urusi ya Usoviet walianza kufanya maandamano ya haki ya kupiga kura ambayo walipewa mnamo 1917. Kwa hiyo ni sahihi kusema kuwa chimbuko la siku ya wanawake iliadhimishwa tu na wanaharakati wa kijamaa na nchi za kikomunisti. Ilipofika miaka ya 1960 hususani mwaka 1967 vuguvugu kubwa la wanawake (Feminist movement) walianza kuitumia siku hii kuadhimisha siku ya wanawake.

Taasisi ya HAKIARDHI imefanya uchambuzi wa bajeti ya Wizara ya ardhi

Taasisi ya HAKIARDHI imefanya uchambuzi wa bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya mwaka 2020/21 ili kubaini ni kwa kiasi gani bajeti hiyo inakidhi mahitaji ya wazalishaji wadogo hususani wanawake katika upatikanaji wa ardhi, matumizi, umiliki na utatuzi wa migogoro ya ardhi.

 

Mradi wa Ardhi Yetu

Taasisi ya Utafiti na Utetezi wa Haki za Ardhi (LARRRI/HAKIARDHI)  ni Taasisi ya Kiraia iliyoanzishwa mwaka 1994 kwa lengo la kufanya Utafiti na Utetezi wa haki za ardhi kwa Wazalishaji Wadogo wadogo nchini ili kukuza uelewa wao katika Sera na Sheria za ardhi na kuimarisha mifumo ya usimamizi, matumizi na utatuzi wa migogoro ya ardhi. HAKIARDHI ilisajiliwa chini ya Sheria ya Makampuni Sura ya 212  mwaka 1994 na kisha mwaka 2019 usajili ulihamishwa chini ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali kwa usajili namba 00NGO/R2/00012.