Skip to main content
x

Taarifa kwa umma: yahusu mradi wa kukuza usalama wa umiliki wa ardhi na rasilimali nyingine kwa wazalishaji wadogo

Taasisi ya Utafiti na Utetezi wa Haki za Ardhi (LARRRI/HAKIARDHI) ni asasi ya Kiraia iliyoanzishwa mwaka 1994 na mwaka 2019 ikasajiliwa kwa usajili namba 00NGO/R2/00012 chini ya Sheria ya Asasi za Kiraia ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019. 

Lengo la kuanzishwa kwa HAKIARDHI ni kufanya utafiti na utetezi wa haki za ardhi kwa wazalishaji wadogo nchini ili kukuza uelewa wao katika utekelezaji wa Sera na Sheria za ardhi ili kuimarisha mifumo ya usimamizi, upatikanaji, mipango ya matumizi na utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Mnamo Machi 22, 2021 HAKIARDHI ilisaini mkataba wa ufadhili na Shirika la Rosa Luxemburg Stiftung kwa lengo la kutekeleza mradi unaofahamika  kwa jina la "Kukuza Usalama na Uhakika wa Umiliki wa Ardhi na Rasilimali nyinginezo kwa Wazalishaji Wadogo".  

Mradi huu ni wa kiasi cha fedha za kigeni Euro 50,000 sawa na TSH. 140,610,000/= na utatekelezwa kati ya mwezi Machi 2021 hadi Disemba 2021.