Skip to main content
x
Mradi wa kuimarisha mfumo wa kidigitali wa taasisi ili kutoa nafasi kwa jamii kupata taarifa za masuala ya ardhi na mabadiliko ya tabianchi

Mradi wa kuimarisha mfumo wa kidigitali wa taasisi ili kutoa nafasi kwa jamii kupata taarifa za masuala ya ardhi na mabadiliko ya tabianchi

Taasisi ya HAKIARDHI ni Asasi ya Kiraia iliyoanzishwa mwaka 1994 chini ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2002 kwa usajili namba 00NGO/R2/00012 wa mwaka 2019.  

HAKIARDHI ilianzishwa kwa lengo la kufanya Utafiti na Utetezi wa haki za ardhi kwa wazalishaji wadogo nchini ili kukuza uelewa wao katika kutetea haki za ardhi ambazo ni kupata, kutumia na kumiliki ardhi. Vilevile, Taasisi hushirikisha jamii za Wazalishaji wadogo taarifa mbalimbali za masuala ya ardhi na mabadiliko ya tabia nchi ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi na ya wakati kuhusu shughuli zao za uzalishaji zinazotegemea ardhi.

Mnamo Disemba 22, 2022 HAKIARDHI ilisaini mkataba wa ufadhili na Shirika la HORIZONT3000 kwa lengo la kutekeleza mradi unaofahamika kwa jina la "Kuimarisha Mfumo wa Kidigitali wa Taasisi ili kutoa nafasi kwa Jamii kupata Taarifa za masuala ya Ardhi na Mabadiliko ya Tabianchi".  

Bajeti ya mradi huu ni Euro 45,332.92 ambazo ni sawa na Tsh. 108,798,960/= na utatekelezwa kati ya mwezi 01 Januari 2023 hadi 30 Novemba 2024.

 

Imetolewa na uongozi wa Taasisi.