Skip to main content
x
LARRI

Taarifa kwa umma: Mradi wa kukuza haki za umiliki wa ardhi kwa wanawake na wakulima wadogo kwa ajili ya maisha endelevu

Taasisi ya HAKIARDHI ni Asasi ya Kiraia iliyoanzishwa mwaka 1994 chini ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2002 kwa usajili namba 00NGO/R2/00012 wa mwaka 2019.  

HAKIARDHI ilianzishwa kwa lengo la kufanya Utafiti na Utetezi wa haki za ardhi kwa wazalishaji wadogo nchini ili kukuza uelewa wao katika kutetea haki za ardhi ambazo ni kupata, kutumia na kumiliki ardhi. Vilevile, Taasisi hushirikisha jamii za Wazalishaji wadogo taarifa mbalimbali za masuala ya ardhi na mabadiliko ya tabia nchi ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi na ya wakati kuhusu shughuli zao za uzalishaji zinazotegemea ardhi.

Mnamo Januari 30, 2023 HAKIARDHI ilisaini mkataba wa ufadhili na Shirika la HORIZONT3000 kwa lengo la kutekeleza mradi unaofahamika kwa jina la "Kukuza haki za umiliki wa ardhi kwa wanawake na wakulima wadogo kwa ajili ya maisha endelevu".  

Bajeti ya mradi huu ni Euro 379,500.00 ambazo ni sawa na Tsh. 1,005,675,000/= na utatekelezwa kati ya mwezi 01 Januari 2023 hadi 31 Disemba 2026.

 

Imetolewa na uongozi wa Taasisi.